The House of Favourite Newspapers

Maalim Seif Akagua Daraja la JPM, Atia Neno – Video

0

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, amewataka Watanzania kulinda miradi inayojengwa katika maeneo ya, ili kupunguza changamoto zinazojitokeza kutokana na ukosefu wa miundombinu husika.

Ametoa rai hiyo wakati akielekea wilayani Chato mkoani Geita,  alipotembelea ujenzi wa mradi wa Daraja la Magufuli (Kigongo – Busisi) linalopita Ziwa Victoria lenye urefu wa mita 3.2, upana wa mita 28.45 na barabara unganishi yenye urefu wa mita 1.66 linalojengwa mkoani Mwanza kwa gharama ya bilioni 700 kwa fedha za serikali ya Tanzania.

 

Aidha, alipongeza juhudi zinazoendelea katika ujenzi huo ambao ni jitihada kubwa za kimikakati ya kuiweka Tanzania katika hali ya kimaendeo, kuwa na wananchi walio na uchumi mzuri kulingana na miundombinu inayojengwa na serikali.

Maalim Seif akisalimiana na Mkuu wa wilaya ya Misungwi, Juma Sweda, ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongela.

“Nampongeza Rais John Magufuli kwa kuona umuhimu wa kujenga daraja hili kwa ajili ya kuunganisha mikoa ya Tanzania na nchi mbalimbali,mradi huu mkubwa ni wakimkakati ukimalizika Watanzania watanufaika, hivyo tuombe dua kwa Mungu wetu ili umalizike haraka,” alisema Maalim.

 

Akitoa taarifa ya ujenzi wa daraja hilo, Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara (Tanroads) Mkoa wa Mwanza, Vedastus Maribe, alisema: “Daraja hilo linajengwa kwa lengo la kuunganisha barabara kuu ya Usagara, Sengerema na Geita katika Ziwa Victoria, ambazo ni sehemu ya barabara zilizoko kwenye ushoroba wa Ziwa Victoria, ambao unaanzia Sirari mpakani na Kenya hadi Mutukula mpakani na Uganda (KM 774) na ushoroba huu unaunganisha mikoa ya Mara, Simiyu, Mwanza, Geita, Kigoma na Kagera.

“Aidha ushoroba huu unaunganisha nchi jirani za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Rwanda, Burundi, Uganda na Kenya, ambapo  daraja hilo linatarajiwa kuchochea maendeleo ya ukanda huu pamoja na Taifa kwa ujumla.

 

“Baada ya kukamilika kwa ujenzi wa daraja hili inategemewa muda wa kuvuka Ziwa Victoria katika maeneo ya Kigongo na Busisi utakuwa takribani dakika nne na idadi ya magari yatakayotumia barabara hii inategemea kuongezeka hadi kufikia magari 10,200 kwa siku na kuondoa uwezekano wa kutokea vifo vingi katika maeneo hayo vitokanavyo na ajali za vyombo vya kuvukia katika maeneo hayo.”

Na Leah Marco, MWANZA

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers)

Leave A Reply