The House of Favourite Newspapers

MAAMUZI WALIYOYACHUKUA BASATA KWA DIAMOND NA RAYVANNY

 

Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), limemruhusu msanii Naseeb Abdul ‘Diamond’ na Raymond Mwakyusa ’Rayvanny’ kufanya maonyesho yao nchini Kenya na Comoro ingawa rufaa yao itajadiliwa Februari mwakani.

 

Katika ratiba zake, Diamond na wasanii wake wataendelea na onyesho la Tamasha la Wasafi  ambapo leo Desemba 24 watakuwa katika mji wa Embu, kabla ya kuhamia jiji la Mombasa Desemba  26 na kuelekea Comorro kwa shoo ya Desemba 28 na kumalizia Nairobi Desemba 31, 2018.

 

Diamond na Rayvanny walifungiwa Desemba 18, 2018 kutofanya maonyesho ndani na nje ya nchi kwa muda usiojulikana wakituhumiwa kufanya makosa mbalimbali tangu kuanza kwa Tamasha la Wasafi ikiwemo kuimba wimbo wa Mwanza ambao umefungiwa.

 

Pamoja na hilo siku tatu zilizopita waliendelea kutangaza kuendelea na maonyesho hayo pamoja na Basata kueleza hawajawaruhusu.

 

Katibu wa baraza hilo, Godfrey Mngereza amesema sababu ya kuwaruhusu ni baada ya kikao kilichoketi siku ya jana na kujadili maombi yao kuomba kusamehewa huku moja ya jambo walilolibaini ni kwamba wasanii hao walikuwa wameshaingia mkataba wa kufanya maonyesho hayo kabla ya kupewa adhabu.

Comments are closed.