The House of Favourite Newspapers

Mabegi ya Barbara Yamshtua Magori

0

WAKATIwakiwa kwenye harakati za kukwea pipa jana kuelekea nchini Misri kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi, mabegi ya Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez yalimvunja mbavu aliyekuwa Mtendaji wa Simba, Crescentius Magori.

 

Barbara aliripoti Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere majira ya saa 7:45 mchana na kupokelewa na Magori ambaye alianza kwa kucheka.

Magori alikuwa akitazama mzigo aliokuwa amebeba Barbara ambao ulikuwa na mabegi manne, matatu makubwa na moja lilikuwa dogo.Magori alisikika akisema kuwa: “Hahaha mabegi yote hayo uliyobeba hakika una jambo lako.”

Stori: Lunyamadzo Mlyuka na Musa Mateja

Leave A Reply