The House of Favourite Newspapers

Mabingwa Burundi Kuwanoa Yanga

KATIKA kuhakikisha wanakuwa fiti kuelekea mchezo wao wa kirafiki dhidi ya AS Vita ya DR Congo, Yanga itavaana na mabingwa wa Burundi, Aigle Noir Makamba FC, Julai 27, mwaka huu kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

 

Yanga itacheza mechi ya kirafiki na AS Vita Agosti 4, mwaka huu ikiwa ni kilele cha Siku ya Mwananchi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar lengo kubwa likiwa ni kuwatambulisha wachezaji wao wapya na wa zamani ambao watakuwa nao msimu ujao.

Kwa sasa Yanga ipo kambini mjini Morogoro ikijiandaa na msimu mpya wa ligi kuu, Ligi ya Mabingwa Afrika na michuano mingine ambayo wanatarajiwa kushiriki.

 

Ikiwa Moro, Yanga imeshacheza mechi mbili za kirafiki ambazo ni dhidi ya Tanzanite ambayo waliichapa mabao 10-1 na jana asubuhi walicheza na Moro Kids na kushinda 2-0.

 

Kaimu Katibu wa Yanga, Dismas Ten, alisema kuwa, maandalizi yanakwenda vizuri mpaka sasa na vijana wanaendelea na programu ambayo aliituma Kocha Mkuu Mwinyi Zahera kwa msaidizi wake, Noel Mwandila.

 

“Tunacheza mechi ya kirafiki na mabingwa wa Burundi ambao ni Aigle Noir, mchezo utapigwa Morogoro Julai 27, ikiwa ni sehemu ya maandalizi yetu.

 

“Pia tutakuwa na mchezo mwingine dhidi ya Mawenzi Market Julai 28, kwenye Tamasha la Faith Baptist Church ambalo nalo litafanyika hapa Morogoro na hakutakuwa na kiingilio hii ni kama sehemu ya shukrani kwa timu ya wananchi.

 

“Hizi ni baadhi ya mechi ambazo ni za maandalizi ambazo mwalimu alipanga kucheza mechi tano pamoja na ile ambayo itakuwa maalum ya Agosti 4, mwaka huu,” alisema Ten ambaye ni miongoni mwa matunda ya vipaji vya Global Publishers iliyoko Sinza Mori jijini Dar es Salaam.

JOEL LWAGA: Niliumwa Hadi Kupooza /Kuhusu MUNA “no comment”

Comments are closed.