The House of Favourite Newspapers

Machinjio ya Vingunguti Kufunguliwa Kesho

0

5

Machinjio ya Vingunguti yaliyofungwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa Nchini (TFDA) kwa zaidi ya mwezi mmoja yanatarajiwa kufunguliwa siku ya Jumatatu baada ya kufanyika ukarabati madhubuti ulioambatana na uwekaji wa miundombinu.

Ukarabati wa machinjio hayo yaliyokuwa yamefungwa kutokana na uchafu uliokithiri pamoja na kuhatarisha afya za walaji nyama umegharimu kiasi cha Shilingi milioni 85.

Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Saidi Kumbilamoto pamoja na Maafisa Afya na Mifugo wametembelea na kukagua machinjio hayo na kujionea uboreshwaji mkubwa wa miundombinu ya kupitishia maji, ujenzi wa makaro mapya, uwekaji wa mabomba ya maji pamoja na hokey mpya kwa ajili ya kuchinjia ng’ombe.

Akizungumza mara baada ya ukaguzi huo, Meya Kumbilamoto amesema tayari Ofisi ya Manispaa imefuatilia TDFA ambapo wanatarajia kupeleka barua rasmi ya kukamilika kwa ukarabati huo ambao kwa kiasi kikubwa umesababisha upungufu wa nyama pamoja na kupanda kwa bei ya nyama katika Jiji la Dar es Salaam.

Credit: Hivisasa

Leave A Reply