The House of Favourite Newspapers

Madai! Familia Yamsusa Mke wa Majuto & Watoto Waike, Asimulia – Video

ZIKIWA zimepita siku chache tangu aliyekuwa msanii mkongwe wa filamu nchini, Amri Athuman ‘King Majuto’ afariki dunia, imedaiwa kuwa, familia ya marehemu mumewe imekataa kumhudumia aliyekuwa mkewe, (Kizuka) Bi. Aisha Mbwana pamoja na watoto wake.

 

Akizungumza na Global TV Online, Bi. Aisha amesema kitendo hicho kimemuumiza na kuamua kufungasha virago vyake kutoka Tanga na kurudi nyumbani kwa wazazi wake, Vingunguti jijini Dar es Saalam.

 

“Baada ya kumaliza kuzika, familia za pande mbili zilikaa kikao na kuubaliana kwamba familia ya mume wangu watakuwa wananihudumia, lakini baada ya muda walibadilika na kukataa, kutoa huduma kwangu na watoto wangu.

 

“Walisema nitumie pesa nilizopewa kama pole niweze kujihudumia na watoto wangu. Mimi nilikubali maamuzi yao, na tangu msiba huo sijawaona, wazazi wangu wameamua kunichukua na kunileta nyumbani Dar es Salaam, lakini namwachia Mungu atasimamia haki za watoto wangu,” amesema Bi. Aisha.

Msikie Mke wa Majuto Akisimulia

Comments are closed.