The House of Favourite Newspapers

Madawa Ya Binadamu Yatupwa Kwenye Makazi

ded-ubungo-7Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo, John L. Kayombo.ded-ubungo-6…Sehemu ya madawa yaliyotupwa.ded-ubungo-1…Mkurugenzi akisisitiza jambo.

Kampuni ya Indepth Scientific inayojihusisha na usambazaji wa madawa ya binadamu na vifaa tiba yenye makao yake mtaa wa Rose Mikocheni jijini Dar es Saalam, viongozi wake wametiwa mbaroni baada ya kubainika wametupa dawa za kutibu maradhi ya binadamu kwenye makazi ya watu.

Chanzo chetu kimezungumza na Global Digital na kusema:

“Mimi ni mkazi wa hapa Mpiji Majohe, Jumatano wiki iliyopita tuliona gari likimwaga takataka hapa, tukashtuka kwasababu siyo eneo la kutupa takataka, wakati bado wanamwaga tulifika na kuwazuia na tulipokagua tukaona ni madawa ya binadamu ya aina tofauti.

“Tulimpigia simu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo bwana , ambaye alifika eneo la tukio akiwa na askari na kuwahoji  dereva na mkuu wa msafara waliotambulika kwa majina ya Mzee Ali na Amosi ambao walijitetea kwa kusema wametumwa na meneja wao, Risper Monyangi.

“ Mkurugenzi akaamuru meneja huyo aje eneo la tukio, baada ya kufika na kubanwa na maswali alishindwa kujitetea na wote watatu walipelekwa kituo cha    Polisi cha Mbezi kwa Yusuph na kufunguliwa Mashtaka.”

Alipotafutwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema:

“Ni kweli tukio limetokea na niwashukuru sana wakazi wa Mpiji Majohe kwa kunipa taarifa, nimesikitishwa sana na kitendo cha kampuni hii kumwaga madawa kwenye makazi ya watu kwa makusudi kabisa wameamua kuwaumiza raia wema na ili iwe mfano na fundisho ni lazima hatua kali zichuliwe dhidi yao.”

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, ACP Suzan Kaganda amesema:

“Bado tunaendelea na uchunguzi na watuhumiwa watafikishwa mahakamani muda wowote kuanzia sasa kujibu mashtaka yanayowakabili.”

 

Comments are closed.