The House of Favourite Newspapers

MADEE HACHUKII CHONGE KUFANANISHWA NA MAI ZUMO

 

MKALI  wa  Bongo Fleva, Hamad Ally ‘Madee’ ameweka wazi kwamba hachukii kuona watu wakimfananisha binti yake, Chonge na mchekeshaji Mai Zumo kwani ni jambo la kawaida.

 

Madee, akipiga stori mbili-tatu na Ijumaa Showbiz alifunguka: “Nimekuwa nikiona mara nyingi watu

wakimfananisha binti yangu Chonge na huyu mtoto mchekeshaji Mai Zumo, ni kweli wanafanana na huwa sichukii kwa sababu ni jambo la kawaida.

 

Pia duniani watu wawiliwawili, hivyo Mungu akitujalia, basi itabidi wafanye kitu cha pamoja ili tutengeneze pesa.”

 

Chonge na Mai Zumo mara kadhaa wamekuwa wakifananishwa kwenye mitandao ya kijamii kutokana na sura zao kufanana.

Comments are closed.