The House of Favourite Newspapers

MGALU, VULLU WAUNGA MKONO KAMPENI YA TOKOMEZA ZERO KISARAWE

Mbunge wa viti maalum CCM mkoa wa Pwani Mh. Zainab Vulu na Naibu Waziri wa Nishati Mh. Subira Mgalu wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali baada ya kukabidhi vifaa  wilaya ya Kisarawe.
Mbunge wa viti maalum CCM mkoa wa Pwani Mh. Zainab Vulu na Naibu Waziri wa Nishati Mh. Subira Mgagalu wakimkabidhi vifaa mbalimbali mkuu wa wilaya ya Kisarawe ikiwa ni kuunga mkono kampeni ya “Tokomeza Zero” wilayani humo.
Mbunge wa viti maalum CCM mkoa wa Pwani Mh. Zainab Vulu akizungumza katika kikao cha RCC kinachoendelea wilayani Kiswarawe wakati akitangaza utekelezaji wa msaada ambao wabunge hao waliuahidi katika ziara ya Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan wakati alipofanya ziara yake

 

WABUNGE wa viti maalum mkoani Pwani ,Subira Mgalu na Zainab Vullu wamechangia magodoro 20 ili kupunguza changamoto ya upungufu wa magodoro uliopo shule ya sekondari Maneromango. Aidha Subira ametoa tanki la maji la lita 2,000 litakalosaidia kuhifadhi maji katika shule hiyo na tanki jingine shule ya sekondari Kolesa iliyopo kata ya Vikumburu.

 

Wakikabidhi msaada wa magodoro na matanki hayo ya kuhifadhi maji, walisema, msaada huo ni sehemu ya kuunga mkono kampeni ya Tokomeza Zero iliyoanzishwa hivi karibuni na mkuu wa wilaya Kisarawe Jokate Mwegelo. “Tumejichanga kila mmoja magodoro kumi, kumi na kwa upande wa maji,mimi nipo karibu na shule ya Maneromango hivyo nimewataka wachote maji kwangu buree “alisema Zainab.

 

Alieleza, wanafunzi wa kike wanahitaji zaidi maji hivyo kwa hakika kwa misaada hiyo itawasaidia kwa kiasi kikubwa. Zainab ,aliwaomba wadau wengine wajitokeze kuchangia katika tokomeza zero, ili kufikia malengo ya kiwilaya kuinua taaluma. Nae Subira alisema ,wazazi na walezi waelekeze nguvu zao kushirikiana na viongozi na serikali kusimamia watoto kuongeza ufaulu.

“Fuatilieni watoto, kufuatilia maendeleo ya kimasomo kwa wanafunzi wetu, tusiachie walimu, tusijisahu wajibu wetu,”:Mkoa na wilaya imejikita kuinua sekta ya viwanda, kama hatutoelimisha watoto jitihada hizo zitakuwa kazi bure “alifafanua Subira.

 

Subira alimpongeza Jokate kwa kufanya vizuri kwa kampeni hiyo kubwa.

Awali Jokate alibainisha, tangu kuanza kwa kampeni ya Tokomeza Zero, tayari wamejenga madarasa kumi na bweni moja kata ya Kurui kwa zaidi ya sh. mil. 100.

 

NA MWAMVUA MWINYI, KISARAWE .

Comments are closed.