The House of Favourite Newspapers

Madega Achukua Fomu Ya Urais TFF, Apambane Na Jamal Malinzi

0
Mwenyekiti wa zamani wa Klabu ya Yanga, Iman Madega

Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) unatarajiwa kufanyika Agosti 12, mwaka huu mkoani Dodoma, habari mpya ni kuwa Jamal Malinzi ambaye ni rais wa sasa wa shirikisho hilo amechukua fomu ya kutetea nafasi yake lakini amepata mpinzani.

Muda mfupi baada ya Malinzi kuchukua fomu ya kutetea nafasi yake hiyo, ndipo mwenyekiti wa zamani wa Klabu ya Yanga, Iman Madega naye akatinga maguu kwenye ofisi za shirikisho hilo kwa ajili ya kuchukua fomu ya kuwania urais wa TFF.

Madega amechukua fomu hiyo leo asubuhi katika ofisi za shirikisho zilizopo Karume jijini Dar es Salaam, hiyo ni dalili njema kwa wanamichezo ambapo awali ilionekana kama Malinzi hatakuwa na mpinzani katika nafasi yake.

Uwepo wa ushindani utaongeza wagombea kuwa na hoja makini mbele ya wajumbe ambao ndiyo wapiga kura.

Leave A Reply