The House of Favourite Newspapers

Mr Universe Atua Bongo, Ashusha Somo kwa Vijana

0
Wasanii walifika Airport kumpokea Mr. Universe.

Mr Universe Tanzania mwaka 2002, Matukio Chuma, amewataka vijana wa Kitanzania kutumia fursa mbalimbali zinazojitokeza ndani na nje ya nchi kuliko kubaki wakilalamika.

Mr. Universe (mwenye miwani) baada ya kuwasili Airport.

Chuma ameyasema hayo, leo wakati akizungumza na wanahabari kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere muda mfupi baada ya kuwasili akitokea Marekani anakofanyia shughuli zake za uandishi wa vitabu, mshairi, ujasiriamali na uhamasishaji.

 

Akizungumza na vyombo vya habari.

“Nashukuru kwa moyo waliouonesha baadhi ya marafiki na ndugu zangu kuja kunipokea. Ushauri na kilio changu kwa vijana wa Kitanzania ni kuthubutu kutumia fursa mbalimbali ambazo zimekuwa zikitangazwa dunianikama ambavyo mimi nilithubutu na ninaendelea kuthubutu,” alisema Chuma.

Msanii wa sinema Bongo, Kojack (kushoto) akiwa na mshkaji wake.

NA:Gabriel Ng’osha/GPL

VIDEO: Dokii Afunguka Mahusiano Yake na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta

Leave A Reply