The House of Favourite Newspapers

Madenti Chuo Kikuu wazichapa kavukavu wakimgombea mbunge!

0

hqdefault(Picha na maktaba)

Na Mwandishi Wetu, AMANI

DODOMA: Wanafunzi wawili wa chuo kikuu kimoja mkoani Dodoma, hivi karibuni walizichapa kavukavu katika maeneo ya chuoni kwao, wakimgombea mbunge mmoja maarufu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) (jina linahifadhiwa), Amani lina mkanda kamili.

Shuhuda aliyekuwepo wakati wa sakata hilo, alisema awali, wanafunzi hao walikuwa ni mashoga na mara zote mbunge huyo alipomhitaji mpenzi wake, walikwenda pamoja kula bata katika viwanja mbalimbali mjini Dodoma na Dar es Salaam.

“Kumbe mheshimiwa mbunge akamgeukia rafiki mtu, akawa anamchukua bila mwenzake kujua, wakawa wanaendelea na mawasiliano na kukutana kwa siri, sasa siku moja mheshimiwa kapaki gari lake maeneo ya chuo, yule mpenzi wake akaliona gari, akajua amefuatwa yeye, alipokwenda akamkuta shoga yake kajaa tele garini anacheka na jamaa,” alisema shuhuda huyo.

Alisema kwa kuwa muda mfupi kabla wanafunzi hao walikuwa pamoja na hawakuzungumzia kuhusu ujio wa mbunge, rafiki huyo akajua amesalitiwa, ngumi zikaanza kupigwa hapohapo na ili kuzima soo, mheshimiwa akawasha gari na kuondoka zake akiwaacha wakiparurana.

Gazeti hili lilimtafuta mbunge huyo machachari anayewakilisha moja ya majimbo yaliyo Kanda ya Mashariki, lakini mara zote simu yake iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa tuhuma zake kupitia simu ya kiganjani, hakujibu.

Kumekuwa na maelezo kuwa wanafunzi wengi wa elimu ya juu, wamekuwa wakijihusisha kimapenzi na watu ili kukabiliana na ugumu wa maisha, ingawa baadhi yao hufanya hivyo kwa ajili ya kupata vitu vya anasa, zikiwemo simu za gharama.

Hivi karibuni Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, alisema wanafunzi wa vyuo vikuu, wanaongoza kwa kujihusisha na biashara ya kujiuza kwa ajili ya kupata hela za matumizi ya anasa. Alitoa kauli hiyo akiwa katika Chuo Kikuu cha Mzumbe kilichopo mkoani Morogoro.

Leave A Reply