The House of Favourite Newspapers

Madhara ya magonjwa ya zinaa kwa wajawazito, watoto

KATI ya maradhi nane ya zinaa, manne yanatibika, nayo ni kaswende, kisonono, chlamydia na trichomoniasis.  Mengine manne yanayosaba­bishwa na virusi na hayana tiba ambayo ni hepatitis B, HIV, herpes simplex virus na human papilloma virus HPV. Maradhi haya huambukizwa hasa kwa njia ya ngono zembe na kusababisha madhara makubwa kwa mjamzito. Madhara ya kaswende kwa mama na mtoto wakati wa ujauzito yapo mengi. Ugonjwa huu ni tishio na husababishwa na bakteria anayeitwa trepone­ma pallidum.

Kaswende wakati wa ujauzi­to unaweza kuwa hatari kubwa kwa kiumbe kilichopo tumboni kwa kukifanya kutoumbika vizuri (deformity) na kifo. Ugonjwa mwingine ni kisonono. Ni miongoni mwa maradhi ya zinaa yanayosaba­bisha bakteria wafahamikao kisayansi neisseria gonorrhoeae (gono). Bakteria hawa husham­bulia utando telezi unaozunguka sehemu za siri.

Kwa wanawake, maambukizi hutokea katika mrija wa urethra, sehemu za siri au mlango wa uzazi (cervix). Ingawa muwasho una­otokana na majimaji katika sehemu za siri unaweza kuwa mkubwa, mara nyingi dalili hizi huwa ni chache au hazitokei kabisa katika hatua za awali.

Kisonono isiyotibiwa in­aweza kusababisha PID (Pelvic Infiammatory Disease) kwa wanawake. Watoto wanaoza­liwa na mama wenye kisonono huwa na hatari ya kuambukizwa wakati wa kuzaliwa; maambuki­zo haya yanaweza kusababisha maradhi ya macho na meno kwa watoto wachanga. Ugonjwa mwingine ni klamid­ia; ni ugonjwa wa kuambukiza unaosababishwa na bakteria wanaoitwa kisayansi chlamydia trachomati. Ugonjwa huo huwa hauoneshi dalili za wazi kwa karibia asilimia 75.

Hivyo, wanawake wengi wenye maambukizi hushindwa kubaini mapema. Wakati dalili zinapoanza kujitokeza, kwa upande wa wanawake huanza kutokwa damu nje ya kipindi chao cha hedhi, maumivu wakati wa kukojoa, kutokwa usaha sehemu za siri au mau­mivu chini ya kitovu.

Kama utaachwa bila kutibiwa hususan kwa wanawake, kla­midia unaweza kuleta madhara makubwa kwake na kwa mtoto.

Huharibu tishu za uzazi za mwanamke na kusababisha uvimbe katika fupanyonga (Pel­vic Inflammatory Disease -PID). PID inaweza kusababisha mauvimu makali katika fupan­yonga, utasa au ugumba au utata katika ujauzito ambao unaweza kusababisha kifo.

Watoto waliozaliwa na mama aliyeambukizwa klamidia huwa na hatari ya kupata upofu au maambukizi katika mapafu. Ugonjwa mwingine wa zinaa hatari kwa watoto ni trikomona­si; husababishwa na maam­bukizi ya protozoa anayefa­hamika kisayansi trichomonas vaginalis. Ugonjwa huu husababisha muwasho na karaha katika uke. Kwa mjamzito unaweza kum­sababishia akajifungua mtoto jiti na maambukizi kwa mtoto baada ya kujifungua.

Ukimwi ambao ni ukosefu wa kinga mwilini, ni matokeo ya maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) -Human Immuno­deficiency Virus (HIV). Ukimwi ni ugonjwa wa zinaa hatari na usiotibika ambao hushambulia mfumo wa kinga ya mwili na kumwacha mgonjwa akiwa hana uwezo wa kujikinga dhidi ya maambukizi madogo.

Wakati wenye VVU wanaweza kueneza kwa njia nyingine, kujami­iana ndiyo njia hasa ya maam­bukizi ya virusi hivi. Wanawake ambao wameathiri­ka na Virusi Vya Ukimwi wanawe­za kumwambukiza mtoto wakati wa ujauzito, kujifungua au mara kadhaa wakati wa kuwanyonye­sha.

Bila matumizi ya dawa za kupunguza makali ya Virusi Vya Ukimwi ni kwa asilimia 15 hadi 30 mtoto anaweza kuzaliwa akiwa na maambukizi ya VVU, asilimia 5 hadi 20 kupata maambukizi wakati wa kunyonyeshwa.

Maradhi mengine ni yale ya­nayosababishwa na virusi kama Human Papilloma Virus ambayo huweza kusababisha saratani ya shingo ya kizazi, maradhi katika mfumo wa hewa wa mtoto na matatizo wakati wa kujifungua.

Hepatitis B, huambukizwa kwa njia ya ngono zembe na maam­bukizi kwa mtoto wakati wa kuji­fungua. Mtoto anapozaliwa ndani ya saa moja baada ya kuzaliwa anaweza kuwa na asilimia 90 ya kupona endapo alizaliwa nao. Herpes huambukizwa wakati wa ujauzito na inaweza kuporomosha ujauzito katika miezi mitatu ya mwanzo.

TIBA

Magonjwa ya zinaa yanati­bika iwapo yatatibiwa mapema isipokuwa Ukimwi ambao bado hauna tiba. Mambukizi mengine mjamzito atatibiwa kwa kupewa antibiotic. Iwapo mtoto ataathirika kipindi mama yake ana mimba, baada ya kuzaliwa atatibiwa na kupona. Kwa ushauri zaidi wasil­iana nasi.

Comments are closed.