The House of Favourite Newspapers

Madiwani Watakiwa Kuachana na Migogoro

0

Buchosa, Sengerema. Madiwani wa Halmashauri ya Buchosa Wilayani Sengerema, Mkoa wa Mwanza wametakiwa kuachana na migogoro ambayo inadidimiza maendeleo ya Wananchi badala yake wawe wazalendo katika suala zima la usimamizi wa masilahi ya umma.

 

Kauli hiyo imetokewa na Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Senyi Ngaga kwenye mafunzo elekezi juu ya uendeshaji wa Halmashauri kwa madiwani wa Halmashauri ya Buchosa ambapo amewakilishwa na Katibu tawala wa Wilaya ya Sengerema, Allen Augustine.

 

Amesema madiwani watumie mafunzo haya kuwasidia kusimamia masilahi ya umma na kuachana na migogoro ambayo inarudisha nyuma maendeleo ya wananchi.

” Tunapaswa kuwa wazalendo na kusimamia masilahi ya umma na ili Halmashauri zetu zisinge mbele mafunzo haya yatakiwa chachu ya maendeleo kwenye maeneo yenu ” amesema Ngaga.

 

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Buchosa Paul Malala amesema wameona nivema kutoa mafunzo hayo kwa madiwani lengo nikuwajengea uwezo kutambua majukumu yao na kuondoa migogoro isiyo ya lazima.

 

Oscar Tandula nimwezeshaji toka ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Mwanza amesema katika mafunzo hayo madiwani wanafundishwa juu ya kaununi za kudumu za uendeshaji wa Halmashauri, sheria ya maadili ya Viongozi wa umma na 13ya mwaka 1995na kanunu za Sheria ya maadili ya Viongozi wa Umma ,udhibiti wa migongano wa masilahi za mwaka 2020.

 

Sambamba na mahusiano ya kisheria Kati ya Serikali kuu na serikali za mitaa ,wajibu ,Majukumu ,haki na stahiki za madiwani pamoja na wajibu wa Diwani katika kuibua ,kupanga na kutekeleza miradi ya maendeleo.

 

” Tunawapitisha kwenye maada hizi wazielewe zitasaidia kujua majumu yako ya kusimamia Halmashauri yao na kuepuka migogoro isiyo na tija kwa masilahi ya Wananchi” amesema Tandula.

Diwani wa viti maalumu kutoka tarafa ya Kahunda Mwamini Gandama amesema mafunzo hayo waliyopata yatawasaidia kusimamia vema majukumu yao hasa katika kutekeleza miradi ya maendeleo.

 

Diwani wa Kata ya Nyakalilo Paul Kabugwe amesema tangu wachanguliwe walikuwa bado hawajajua namuna ya kusimamia Halmashauri kama Madiwani hivyo mafunzo haya yamewajengea uwezo hivyo watatimiza majukumu yako ipaswavyo.

 

Usuli

Madiwani 29 wa Halmashauri ya Buchosa Wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza wamepata mafunzo ya kanuni za kudumu za uendeshaji wa Halmashauri yao.

MWANDISHI: DANIEL MAKAKA – BUCHOSA

Leave A Reply