The House of Favourite Newspapers

MADRID, DORTMUND ZATUPWA NJE UEFA

REAL Madrid wameendelea kuandamwa na matokeo mabaya msimu huu baada ya usiku wa kuamkia leo kuchapwa mabao 4-1 na Ajax na kuondolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Madrid wakiwa kwenye dimba lao la Santiago Bernabeu, walikuwa wanajiamini kuwa wanaweza kupata ushindi kirahisi baada ya kushinda mabao 2-1 nchini Uholanzi wiki tatu zilizopita, lakini mambo yakawa magumu.

 

Madrid ambayo imefungwa michezo minne ya hivi karibuni nyumbani kwenye michuano yote ilionyesha kiwango cha chini sana kwenye mchezo huo ikiwa bila ya nahodha wake, Sergio Ramos mwenye adhabu ya kadi za njano.

Kipindi cha kwanza kilitosha kuwapa Ajax matumaini ya kufuzu kwa hatua ya robo fainali baada ya dakika ya saba tu kuwa mbele kwa bao lililofungwa na Hakin Ziyech na dakika kumi baadaye David Neres akatumia uzembe wa mabeki wa Madrid na kuweka mpira kimiani.

 

Ajax walikwenda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 2-0, lakini waliporejea katika dakika ya 62, Dusan Tadic aliifungia bao la tatu ingawa marudio ya kamera yalionyesha kuwa mpira ulitoka kabla ya bao kufungwa lakini mwamuzi alipeleka kati.

Madrid walipambana na kufanikiwa kupata bao moja kupitia kwa Marco Assensio katika dakika ya 70, lakini maajabu yalitokea kwa mabingwa hao watetezi baada ya dakika moja mbele kuruhusu bao la nne lililofungwa na Schone kwa mkwaju wa faulo na kuwafanya Ajax wafuzu kwenda robo fainali kwa ushindi wa jumla wa mabao 5-3. Dakika chacheĀ kabla ya kumalizika kwa mchezo huo, Nacho Fernandez wa Madrid alitolewa uwanjani kwa kuonyeshwa kadi ya pili ya njano iliyofuatia na nyekundu kutokana na kucheza rafu.

SPURS YAFUZU ROBO Katika mchezo mwingine uliokuwa unapigwa nchini Ujerumani, Tottenham Hotspur walifanikiwa kwenda hatua ya robo fainali baada ya kuwachapa Borrusia Dotmund bao 1-0 kwenye Uwanja wa Westfalen. Spurs walifanikiwa kujipatia bao lao pekee kupitia kwa Harry Kane katika dakika ya 48 ya mchezo.

Katika mchezo wa kwanza uliopigwa kwenye Dimba la Wembley nchini England, Spurs walishinda mabao 3-0 na hivyo wamekwenda robo fainali kwa ushindi wa mabao 4-0.

MAN UNITED LEO Kocha wa zamani wa Manchester United, Alex Ferguson aliondoka na msafara wa timu hiyo jana kwenda Ufaransa ambapo leo watavaana na PSG. Katika mchezo wa kwanza uliopigwa kwenye Dimba la Old Traļ¬€ ord, United walichapwa mabao 2-0 na leo wanatakiwa kushinda mabao 3-0 ili kufuzu kwa hatua ya robo fainali. Mechi nyingine ya leo ni Porto dhidi ya AS Roma.

Comments are closed.