The House of Favourite Newspapers

MAELFU WALIVYOIPOKEA SOKABET MTAANI SIKU YA YANGA VS SIMBA

0
Wasanii wakitumbuiza kwenye promotion ya Sokabet
Mwakilishi wa Sokabet akimuelekeza jinsi ya kubet mmoja kati watu waliohudhuria kwenye promotion hiyo

 

 

MAELFU ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, jana Jumamosi walijipatia elimu ya kubadili maisha yao kwa kubashiriki matokeo, shughuli iliyofanyika siku ambayo kulikuwa na mchezo wa Yanga dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar.

 

Mchezo huo wa Ligi Kuu ulikuwa na presha kubwa na hiyo ikasababisha idadi kubwa ya mashabiki kuwa katika presha pia ya kuona timu gani itaibuka na ushindi lakini mwisho wake matokeo yakawa sare ya bao 1-1.

Elimu hiyo ilitolewa na Kampuni ya Sokabet ambayo ilizunguka mitaa mbalimbali ya Dar kupata maoni yao juu ya Sokabet pamoja na kutoa elimu kkwa washiriki ambao wanatakiwa kuanzia umri wa miaka 18.

Akizungumzia promosheni hiyo ya kipekee ambayo iilihusisha vijana waliokuwa wakidansi mitaani kila walipopita wakiwa na fulana za Sokabet, Franco Ruhinda alisema huo ni mwendelezo wa kampuni yao katika kuwafikia washiriki wa kubashiri matokeo moja kwa moja.

Vijana hao waliokuwa wakidansi walikuwa kivutio kwa wananchi wengi waliowaona huku wengi wakihitaji kupata elimu kuhusu mchezo huo ambao unaweza kukupa hadi shilingi milioni 100 kwa shilingi 1,000 tu.

 

Mmoja kati ya waliofanikiwa kupata elimu hiyo ni msanii wa muziki wa Bongo Fleva aliyekuwa memba wa Kundi la Daz Nundaz, Sajo ambaye alionyesha kufurahia kujua huduma za Sokabet ambapo alisema:

 

“Kuanzia sasa nitakuwa nikibeti na Sokabet kwani mkwanja upo njenje. Niombe tu uongozi wa Sokabet wajitahidi kuwajulisha Watanzania wengi kuhusiana na faida ambazo wanaweza kuzipata wakibeti na Sokabet kama nilivyozipata mimi siku ya leo.”

 

Vijana hao walipita hadi mitaa ya Temeke ambapo huko nako walipokelewa vizuri na umati mkubwa wa watu kutokana na wengi wao kuwa kwenye purukushani za kuelekea Uwanja wa Uhuru kulipokuwa kukifanyika mchezo wa Yanga na Simba.

MWANDISHI WETU

 

Leave A Reply