The House of Favourite Newspapers

MAFUNZO YA WAANDISHI HABARI ZA MAHAKAMA YAENDELEA MJINI MOROGORO

Ofisa Tehama kutoka Mahakama ya Rufani-Tanzania, Bw. Allan Machella akitoa mada ya ‘Njia kuelekea Mahakama Mtandao, Mipango na Mafanikio.’
Wakili wa Kujitegemea kutoka Haki Advocates, Bw. Aloyce Komba akitoa Mada ya utoaji wa Habari za Kimahakama kwa Waandishi wa Habari za Mahakama wanaoshiriki katika mafunzo ya Uandishi wa Habari za Kimahakama katika Ukumbi wa Magadu mkoani Morogoro.
Naibu Msajili, Mahakama Kuu, Mhe. Augustino Rwizile akitoa mada ya ‘Hatua mbalimbali za Mashauri ya Jinai na Madai’, lengo ni kuwaelimisha zaidi Waandishi hao juu ya hatua, taratibu mbalimbali katika uendeshaji wa mashauri hayo.
Washiriki wakifuatilia mada kwa umakini akiwemo mwandishi wa habari wa Global Publishers, Denis Mtima (wa nne kulia).
Mwandishi wa Nipashe, Bi. Hellen Mwango akichangia mada katika mafunzo hayo.

MAFUNZO ya waandishi wa habari yaliyoanza jana Mjini Morogoro yameendelea leo katika Ukumbi wa Magadu mkoani Morogoro. Mafunzo hayo  yanahusu namna  ya utoaji wa Habari za Kimahakama kwa waandishi wa habari  juu ya uelewa namna watakavyoweza kuongeza ujuzi wa taaluma yao.

(Picha na Mary Gwera)

Comments are closed.