The House of Favourite Newspapers

Magari Makali ya Bei Nafuu Haya Hapa! – Video

KAMA ilivyo kawaida, Kampuni ya Udalali ya Tambaza Auction Mart and General Brockers Ltd, inakuletea mnada mwingine mkubwa wa hadhara ukihusisha magari na vitu vingine kibao, utakaofanyika katika Bandari Kavu ya Dar es Salaam, Jumamosi hii, Juni 1, 2019.

Magari hayo ni yale yaliyoingizwa nchini kisha wenye nayo wakashindwa kuyalipia kodi hivyo yakataifishwa na Serikali kwa mujibu wa sheria hivyo yanauzwa katika mnada wa wazi baada ya kukamilika kwa taratibu zote za kisheria.

Akizungumza na Global TV Online, Ofisa wa Tambaza Auction Mart, Krotida Mlimila amesema wananchi wote wanaruhusiwa kwenda kukagua bidhaa zote zitakazouzwa kwenye LCDs zilizopo ofisi za LW9, Bandarini, nyuma ya Police Central kuanzia kesho Alhamisi ili siku ya mnada wanunue kirahisi.

Amesma baadhi ya vifaa vitakavyopigwa mnada Jumamosi ni pamoja na magari (Mercedes Benz, BMW n.k), vifaa vya kilimo, ujenzi nondo, tiles, mitumba na vitu kibao. Mnada huo wa aina yake utaanza Jumamosi saa 4:00, Ubungo.

(Kwa Mawasiliano piga 0713 327 989 au 0715 683 777 au 0713 508 158 au nenda ofisini kwao, Sinza Mori).

TAZAMA HAPA NAMNA YA KUNUNUA MAGARI HAYO JUMAMOSI

Comments are closed.