The House of Favourite Newspapers

Maghorofa, Magari ya Lugumi Yapigwa Mnada Dar

0

Mjengo wa Lugumi Mbweni jijini Dar es Salaam.

KAMPUNI ya Udalali ya Yono leo Septemba 9, 2017 imepiga mnada maghorofa yanayomilikiwa na kampuni ya Lugumi. Maghorofa hayo mawili yapo maeneo tofauti moja likiwa Mtaa wa Mazengo Upanga na lingine likiwa Mbweni jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Yono, Scolastica Kevela aliesema leo kuwa wamefanikisha mnada wa kwanza wa nyumba iliyopo Mbweni uliohudhuriwa na watu mbalimbali ambapo wateja walitembezwa kwenye nyumba hizo na kupanga bei tayari kwa mchakato wa kununua.

Lugumi.

Kevela aliongeza kwamba hawezi kutaja gharama halisi ya mali hizo na deni ambalo kampuni hiyo inadaiwa na Mamlaka ya Mapato (TRA).

“Kazi yetu sisi ni kupiga mnada tu, gharama ya deni na thamani ya mali hizo TRA ndiyo wanatakiwa kutolea majibu. Nyumba ya kwanza  imefikia Shilingi 460 milioni lakini bado haijapata mteja,” alisema Kevela nakuongeza kwamba fedha watakazozipata zitakwenda kusaidia nchi katika shughuli mbalimbali za maendeleo.

Shuhudia Maghorofa ya Lugumi Yakipigwa Mnada

Spika Ndugai: Kwa Nini Lissu Hakupelekwa Muhimbili Au Apollo India?

Leave A Reply