The House of Favourite Newspapers

JPM Aeleza Kitwanga Alivyomsumbua Ujenzi wa Barabara -Video

0

MGOMBEA urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM),  John  Magufuli, amekumbuka jinsi aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Misungwi, Charles Kitwanga, alivyomsumbua kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Usagara, ambayo hapo mwanzo haikuwepo.

Mbunge wa Jimbo la Misungwi, Charles Kitwanga.

Ametoa kauli hiyo hii leo Septemba 8, 2020, wakati akizugumza na kumnadi mgombea wa sasa wa Jimbo la Misungwi, Alexander Mnyeti,  katika eneo la Usagara.

“Mimi nataka tu nieleze ukweli; nilikuwa na mbunge hapa Mheshimiwa Kitwanga alikuwa ananisumbua sana baadhi ya miradi.  Nataka kuwaeleza mipango iliyofanyika hapa ni mingi hata hii barabara haikuwepo katika kipindi cha miaka mitano.  Tuliifanya na aliyenisumbua ni Kitwanga.  Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni; alinisumbua sana ujenzi wa barabara hiyo,”  amesema Magufuli.

Leave A Reply