The House of Favourite Newspapers

Magufuli Afunguka Kuhusu Madai ya Kupotea kwa Sh. Trilioni 1.5 – Video

 

Rais Dkt. John Pombe Magufuli amefunguka na kusema kuwa katika ripoti ambayo alipokea kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Prof. Mussa Assad haikuonyesha upotevu wa fedha hizo na kueleza endapo kungebainika kitu kama hicho, basi aliyehusika angechukua hatua kali siku hiyo hiyo. 

 

Magufuli amesema hayo leo April 20, 2018 wakati akiwaapisha Majaji 10, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wakili Mkuu wa Serikali, Naibu Wakili Mkuu wa Serikali na Naibu Mkurugenzi wa Mashitaka, Ikulu Jijini Dar es Salaam na kusema kuwa watu wanatumia uhuru wao vibaya na kupotosha watu kuhusu upotevu wa fedha hizo na kuleta taharuki katika nchi.

 

“Sasa hivi Tanzania kuna ugonjwa tumeupatawa wa kufikiri na kuamini kila kinachoandikwa kwenye mitandao ni cha kweli, nimesoma baadhi ya mambo wengine wanasema serikali imeiba Sh. Trilioni 1.5, nikamuuliza CAG mbona kwenye ripoti yako uliyonisomea hapa Ikulu hukunieleza huu wizi? Hii trilioni 1.5 mbona hamna, sasa hawa wa trilioni 1. 5 uliwaficha wapi? CAG Prof. Assad akanijibu hakuna kitu kana hicho, Katibu Mkuu akasema hakuna hakuna trilioni 1.5 iliyoibiwa na serikali.

 

 

“Sababu ya uhuru wa mtu kuandika chochote, nikacheka tu, hata ndege tuliambiwa ni mbovu, mtu hamuogopi Mungu, anaandika na kuaminisha watu, ningempata hata kama angekuwa Waziri siku hiyo hiyo angeondoka, natafuta hela halafu ziwe zinaibiwa. Lakini kwa vile ipoti ya CAG huwa inajadiliwa kwenye PAC, Wabunge watajadili wataona.

 

“Unapotosha umma wa Wa-Tanzania milioni 55, madhara yake ni makubwa sana, lazima tutangulize maslahi ya nchi yetu mbele, inawezekana kuna watu wanakuchukia wewe Jaji Mkuu ama wananichukia mimi, chuki hii tusiipeleke kwa Watanzania, naamini katika sheria hizi, kesi kama hizi zikija mtazishughulikia haraka haraka.

“Tanzania tunaipenda sote, nchi hii ikiharibika hayupo atakayebaki salama, tunaweza tukafikiri tupo pembeni, lakini madhara yake ni makubwa kwelikweli,” alisema Rais Magufuli.

VIDEO: MSIKIE RAIS MAGUFULI AKIFUNGUKA

Comments are closed.