The House of Favourite Newspapers

Magufuli Akutana na Wanunuzi Wa Korosho Atoa Msimamo Serikali – Video

Rais John Magufuli ametoa msimamo wa Serikali kuwa bei ya korosho isipungue Sh 3000 kwa kilo moja.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo Jumapili Oktoba 28, 2018 alipokutana na wadau na wanunuzi wa korosho katika kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

 

Hayo yamejiri baada ya wakulima wa zao hilo katika mikoa ya Lindi na Mtwara kuingia kwenye mgomo wa kuuza zao hilo la Korosho kwa kile walichokidai kushuka kwa bei ya zao hilo ukilinganisha na miaka miwili iliyopita huku gharama za uzalishaji zikiwa zimepanda.

 

Kufuatia mgomo wa minada ya siku mbili, Oktoba 26, Rais Magufuli, alimuagiza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuwaeleza kuwa anaunga mkono hatua ya maamuzi hayo ya wakulima na kusema yuko nao bega kwa bega.

 

Miongoni mwa viongozi walioshiriki katika kikao hicho ni pamoja na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba na watendaji wengine wa serikali.

 

“Nawataka wafanyabiashara muelewe kuwa, hakuna korosho itakayouzwa chini ya shilingi 3,000. Kama hamtanunua, mniambie.

 

“Serikali tunaunga mkono wakulima kukataa bei za korosho. Ndio maana kiongozi wa Bodi ya Korosho alipowatisha wakulima kuwa lazima wakubali, tumemuondoa, na hatorudi huko.”Amesema Rais Magufuli.

TAZAMA VIDEO HAPA

Comments are closed.