The House of Favourite Newspapers

Simba Yaigaragaza 5-0 Ruvu Shooting, Mabao Yote Yako Hapa – Video

Mchezo Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Timu ya Simba na Ruvu Shooting umemalizika muda huu Uwanja wa Taifa ulianza saa 1:00 Usiku, kwa Simba kuibuka na ushindi mnono wa bao 5-0 ambapo mabao ya Simba yamefungwa na Emmanuel Okwi dakika ya 7 baada ya kupoke pasi kutoka kwa Shomari Kapombe.

 

Dakika ya 23 Simba wakapata bao la pili kutoka kwa Meddie Kagere baada ya Shiza Kichuya kupiga kona iliyogonga mwamba ikakutana na Kagere akafunga bao la 2 lililodumu kwa kipindi chote cha kwanza.

Kipindi cha pili Claytous Chama akamtengenezea pasi nzuri Emmanuel Okwi akapachika bao la tatu dakika ya 56.

 

 

Emmanuel Okwi huyo huyo akamaliza na Hat trieck baada ya kupokea pasi kutoka kwa Shomari Kapombe dakika ya 78 na kuandika bao la nne kabla ya Adam Salamba kufunga ubao wa magoli kwa kufunga bao la tano akipokea pasi kutoka kwa Hassan Dilunga dakika ya 89.

 

Mchezo ulivyoanza, Bwire alikuwepo Uwanjani katika viti vya watu maalum, VIP ,Okwi alipoanza kuandika bao la kwanza dakika ya 7 bado alikomaa akiamini wana nafasi ila bao la tatu lilipofungwa na Emmanuel Okwi dakika ya 56 hakuoneka tena mpaka mchezo unaisha.

Hadi kipenga cha mwisho, Ruvu Shooting 0-5 Simba, dk ya 90 Uwanja wa Taifa.

MAGOLI Yote ya RUVU SHOOTING VS SIMBA 0-5

Comments are closed.