The House of Favourite Newspapers

Magufuli Apiga Marufuku Viongozi wa CCM Kuitwa Waheshimiwa

Rais John Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM),  ameelekeza kuwa ni marufuku kwa kiongozi yeyote wa chama hicho tawala nchini Tanzania kuitwa mheshimiwa, badala yake waitwe ndugu au komredi.

 

Hayo yameelezwa leo Jumatatu Januari 7, 2019 na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Humphrey Polepole wakati akihojiwa katika kipindi cha Power Breakfast kilichorushwa na Redio Clouds.

 

“Nimefarijika kwa jambo moja, mmenitambulisha kama Komredi, kwa Chama cha Mapinduzi viongozi wote kwa sasa hivi mwenyekiti na vikao wameelekeza ni marufuku viongozi wote kuitwa mheshimiwa, wote tunaitwa ndugu au komredi,” amesema Polepole.

Comments are closed.