The House of Favourite Newspapers

Mtuhumiwa Mauaji ya Mwanaharakati wa Tembo Aanguka Mahakamani – Video

0

MSHTAKIWA mmoja katika kesi ya mauaji ya Mwanaharakati wa kupambana na mauaji ya Tembo, Wayne Lotter amezimia mahakamani huku mwenzake akiieleza mahakama kuwa, raia wa kigeni katika kesi hiyo wanaoishi gereza la keko wamenyimwa chakula kwa siku tano na kupelekea hali yao kudhoofu.

 

Mshtakiwa Ndimana Zebadayo ambaye ni raia wa Burundi amedai hayo jana Januari 17,2020 wakati kesi hiyo inayomkabili yeye pamoja na wenzake 17 ilipofika mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa.
Mapema wakili wa Serikali, Easter Martin amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Mfawidhi, Godfrey Isaya kuwa Kesi hiyo leo imekuja kwa ajili ya kutajwa kwani upelelezi bado haujakamilika na jalada la kesi liko kwa DPP.

 

Awali kabla washtakiwa hao walipotakiwa kupanda kizimbani, mshtakiwa Habonimana Nyandwi raia wa Burundi, alishindwa kusimama na kudondoka chini huku akionekana muguruza nacho, ndipo askari polisi waliokuwa katibu walimsogelea na kumvua viatu pamoja na mkanda wa kaptura yake.

 

Kufuatia hali hiyo, washtakiwa wenzake walipanda kizimbani ndipo mshtakiwa Zebadayo akanyoosha mkono huku akiangua kilio kwa nguvu na kudai, raia wa kigeni waliopo kwenye kesi yao hiyo hawajui ushiriki wao lakini hawana ndugu wala mtu yeye wa kuwaona wala kuwapa chakula.

 

“Tumedhoofika hatuna ndugu wa kutuletea chakula hapa nchini na gerezani tunanyimwa chakula leo siku ya tano, tumekatiwa huduma ya chakula kam raia wa kigeni leo.

 

Akijibu hoja hizo, wakili Easter amedai, mahabusu wanapatiwa huduma zote za chakula pamoja na malazi. Magereza, hivyo kuhusu hilo suala ni vema, wakaulizwa Magareza. Ila upelelezi uko hatua za mwisho, jalada lipo kwa Dpp kwa ajili ya kulisoma.

 

Hata hivyo, askari magereza alipoulizwa juu watuhumiwa hao kutolewa chakula alidai kuwa hana taarifa zozote kwa anachojua yeye mahabusu wote wanapata chakula.

 

Naye, mshtakiwa Ayubu selemani amedai, katika mahabusu ya keko kuna raia wa kigeni wengi na Washtakiwa katika kesi hiyo ya mauaji namba 9 ya mwaka 2017 ni raia wa Burundi Habonimana Nyandwi na Nduimana Jonas maarufu Mchungaji (40) mkazi wa Kamenge Burundi,Robert Mwaipyana.

 

Wengine ni Godfrey Salamba (42) mkazi wa Kinondoni Msisiri A. Inocent Kimaro (23) mkazi wa Temeke Mikoroshini, Chambie Ally (32) mkazi wa Kia/Boma na Ofisa wa NBC, Robert Mwaipyana (31) mkazi wa Temeke Mikoroshini. Wengine ni Meneja wa Benki ya Backlays, Khalid Mwinyi (33) mkazi wa Mikocheni B, Rahma Almas (37).

 

Leave A Reply