The House of Favourite Newspapers

Matokeo NECTA 2019: DC Kinondoni Awafanyia Kitu Walimu

0

 

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,  Daniel Chongolo,  akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) kwenye hafla ya kuwapongeza walimu, waratibu wa elimu na maofisa wa elimu wa Manispaa ya Kinondoni kwa matokeo mazuri ya darasa la saba mwaka jana kwa kushika nafasi ya tatu kitaifa. 

 

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo, jana amewapongeza walimu, waratibu elimu na maofisa elimu wa Manispaa ya Kinondoni  kwa matokeo mazuri ya darasa la saba mwaka jana na kushika nafasi ya tatu kitaifa.

Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamini Sitta, akizungumza kwenye hafla hiyo.

 

Chongolo alitoa pongezi hizo jana kwenye hafla  iliyofanyika Ukumbi wa Police Officers Mess, Oyster Bay jijini Dar.

 

Sehemu ya wageni waalikwa wakifutilia yaliyokuwa yakiendelea.

 

Katika hafla hiyo shule zilizofanya vizuri zaidi zilitunukiwa vyeti  na pesa taslimu katika kuwapa moyo wa kuendelea kufanya vizuri zaidi.

 

Chongolo akizungumza na wageni waalikwa.

 

Mkuu huyo wa wilaya aliwapongeza walimu na wadau wote kwa kufanya kazi nzuri pamoja na wakati mwingine kukumbana na mazingira magumu ya kikazi.

 

…Akimpa mkono wa pongezi na cheti mmoja wa waratibu wa elimu kwa niaba ya shule zake.

 

Maofisa wa benki ya NMB na CRDB Bank nao walikuwa sehemu ya wadau wa elimu walioalikwa kwenye hafla hiyo.

 

Mmoja wa walimu ambaye shule yake imefanya vizuri akipokea cheti kwa niaba ya shule yake.

 

Chongolo naye alifanyiwa ‘sapraiz’ na maofisa elimu kwa kupewa tuzo ya kuutambua mchango wake katika sekta ya elimu.

 

HABARI: NEEMA ADRIAN

PICHA: RICHARD BUKOS /GPL

Leave A Reply