The House of Favourite Newspapers

Mahakama 11 Lindi zafungwa

0

Stori: Mwandishi Wetu,  UWAZI

LINDI: Mahakama za Mwanzo 11 kati ya 37 zilizopo mkoani Lindi hazifanyi kazi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya ubovu wa majengo.

Akizungumza na gazeti hili wiki iliyopita, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Lindi, Geofrey Mhini alisema mahakama hizo ni za wilaya tatu mkoani hapa.

Alizitaja wilaya hizo kuwa ni ya Lindi, Nachingwea na Kilwa.

Akitoa mfano katika mchanganuo wake, Hakimu Mnini alisema katika Wilaya ya Lindi zipo mahakama 13 lakini zinazofanya kazi ni saba na Nachingwea kuna mahakama za mwanzo nane lakini zinazofanya kazi ni nne.

Tayari  Wizara ya Fedha na Mipango imetoa sh.bilioni 12.3 kwa ajili shughuli za mahakama ikiwa ni sehemu ya ahadi ya  Rais Dk. John Pombe Magufuli aliyoiahidi katika kilele cha maadhimisho ya  siku ya sheria.

Ahadi ya rais ilitolewa baada ya maombi ya Jaji Mkuu, Othman Chande katika maadhimisho ya kuanza kwa mwaka wa mahakama kudai wana uhaba wa fedha za kuendeshea shughuli za kimahakama.

Leave A Reply