The House of Favourite Newspapers

Mahakama Kuu Yatupilia Mbali Kesi ya Mbatia

0

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali kesi ya Kikatiba iliyofunguliwa na Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia ya kupinga utaratibu wa kujiuzulu kwa aliyekuwa Spika wa Bunge Job Ndugai ambapo hata hivyo Mawakili wa Mbatia wamesema watakata rufaa kupinga uamuzi huo.

 

Uamuzi huo umetolewa leo Januari 28,  na Jopo la Majaji watatu wakiongozwa na Jaji John Mgeta ambapo amesema Ndugai alifata utaratibu wa kujiuzulu ikiwemo kuandika Barua kwa mkono ya kujiuzulu kwenda kwa Katibu wa Bunge huku barua ya pili akaiwasilisha kwa Chama chake kupitia Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

 

Jaji Mgeta amesema ya kwamba hakuna Mtanzania aliyeiona barua ya Spika kujiuzulu bali iliyokuwa ikisambaa ni taarifa kwa umma iliyotolewa na chama chake na si barua ya kujiuzulu ambapo baada ya kueleza hayo, Jaji Mgeta akampatia Mbatia nakala kivuli(Copy) ya barua ya Ndugai alivyojiuzulu.

Leave A Reply