Mahakama Yaamuru Heche, Msigwa, Bulaya, Mdee Wakamatwe

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeamuru wabunge wanne wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakamatwe na kufikishwa mahakamani hapo kwa kukiuka masharti ya dhamana.

 

Wabunge hao ambao ni washtakiwa katika kesi ya uchochezi namba 112 ya mwaka 2018 ni; Ester Bulaya (Mbunge wa Bunda Mjini), John Heche (Mbunge wa Tarime Vijijini), Peter Msigwa (Mbunge wa Iringa Mjini) na Halima Mdee (Mbunge wa Kawe).

 

Amri hiyo imetolewa leo Novemba 15, 2019, na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kufuatia washtakiwa hao kutofika Mahakamani hapo wakati kesi yao ilipokuja kwa ajili ya kusikilizwa ushahidi upande wa utetezi bila ya kuwepo taarifa zozote kutoka kwao wala wadhamini wao.

 

Baada ya kutoa agizo hilo hakimu ameiahirisha kesi hiyo hadi Novemba 21, 22 itakapoendelea na upande wa utetezi kuendelea na ushahidi wao.


Loading...

Toa comment