The House of Favourite Newspapers

Mahakama: Yaamuru Mdee na Wenzake Bado ni Wabunge

0
Wabunge 19 waliovuliwa Uanachama na CHADEMA

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imeridhia wabunge 19 wa Viti Maalum ambao wamevuliwa uanachama na Chadema kuendelea na ubunge mpaka maombi yao ya kibali cha kufungua kesi kupinga uamuzi wa Kamati Kuu ya chama hicho ulioridhiwa na Baraza Kuu wa kuwavua uanachama yatakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.

 

Akitoa maelezo hayo, Jaji wa Mahakama Kuu, John Mgeta jioni ya leo Jumatatu ametoa zuiohi lo la Halima Mdee na wenzake 18 wasiondolewe bungeni hadi kesi ya msingi itakaposikilizwa. Kesi hiyo itaendelea tena Juni, 13 2022.

Spika wa Bunge Dkt. Tulia Akson amesema Bunge haliwezi kuingilia Mahakama juu ya sakata la wabunge 19 wa CHADEMA

Mnamo Mei 12, 2022Baraza Kuu la Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA lilitoa uamuzi wa kuwafuta Uanachama Wabunge hao 19.

 

Jambo hilo lilipelekea mapema leo Mei 16, 2022 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Akson kutolea maelezo na ufafanuzi juu ya sakata la wabunge hao, ambapo alisema jambo hilo lipo mahakamani na Mahakama ndiyo chombo pekee kinachoweza kutoa haki.

 

Leave A Reply