Dkt. Abbas Atembelea Ujenzi wa Kituo cha Michezo cha TFF Tanga
![](https://globalpublishers.co.tz/wp-content/uploads/2022/05/WhatsApp-Image-2022-05-16-at-4.47.19-PM.jpeg)
KATIBU MKUU wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi leo Mei 16, 2022 amekagua ujenzi wa kituo cha kisasa cha michezo kilichopo Kata ya Mnyanjani jijini Tanga kinachojengwa na Shirikikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF).
Katika ukaguzi huo Dkt. Abbas amesema:
![](https://globalpublishers.co.tz/wp-content/uploads/2022/05/WhatsApp-Image-2022-05-16-at-4.47.22-PM.jpeg)
“Ingawa kituo kama hiki cha Dar es Salaam kiko mbele zaidi ya hiki kiutekelezaji lakini hapa pia nimeridhika na maelezo ya wataalamu kuhusu maendeleo ya mradi huu utakaokuwa moja ya miundombinu mingine ya kisasa katika safari ya Serikali ya Awamu ya Sita kushirikiana na wadau kufanya mageuzi katika michezo nchini,” alisema Dkt. Abbasi aliyeambatana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa TFF, Athumani Nyamlani na Mkurugenzi wa Michezo, Yusuph Singo.