The House of Favourite Newspapers

Mahakama Yataka Haki Itendeke Kesi ya Mhasibu Takukuru

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imetaka haki itendeke kuhusu kesi ya kudaiwa kumiliki mali zenye zaidi ya thamani ya Shilingi bilioni 3.6 kinyume na kipato chake halali inayomkabili aliyekuwa mhasibu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Godfrey Gugai,  pamoja na wenzake wawili.

 

Kesi hiyo iliitwa jana Jumatatu, Oktoba 21, 2019 kwa ajili ya kuendelea na ushahidi lakini upande wa mashtaka kupitia Wakili wa Serikali, Sylvia Mitanto,  ulidai kuwa mawakili wa kesi hiyo hawapo.

 

Hakimu Simba alisema hajafurahi kuona kesi hiyo inaahirishwa tena kwa sababu mashtaka yanayowakabili washtakiwa hayana dhamana. Kesi imeahirishwa hadi Oktoba 28, 2019 kwa ajili ya kuendelea na ushahidi.

Comments are closed.