The House of Favourite Newspapers

MAHAKAMA YAWAACHIA HURU WAKURUGENZI WA JAMII FORUMS

 

KESI namba 457 (Jamhuri v Maxence Melo na mwenzake Micke William) inayohusu kampuni za CUSNA Investment na Ocean Link kudaiwa kukwepa kodi Bandarini Dar na kunyanyasa wafanyakazi wa kitanzania imeendelea leo Juni 01, 2018 katika Mahakama ya Mkazi, Kisutu.

Akisoma shauri hilo Hakimu Godfrey Mwambapa amesema washitakiwa hawana kesi ya kujibu na hiyo Mahakama imewaachia huru kuanzia leo. Hili ni moja kati ya mashauri 3 yaliyokuwa yanawakabili washtakiwa. Kwa mantiki hiyo, bado kuna mashtaka 2 yatakayotajwa mahakamani hapa Juni 18.

Kesi hii namba 457 iliyokuwa ikiikabili JamiiForums, ilihusu kampuni ya CUSNA Investment ambayo ilidaiwa kufoji nyaraka bandarini, kukwepa kodi na kuwatesa wafanyakazi wazalendo na kupendelea wageni toka nje ya nchi.

 

Katika kesi hii, Polisi walitaka JamiiForums iwapatie taarifa za mwanzisha mada Kwayu na mchangiaji mmoja AMRISHIPURI ili waweze kuwakamata na kuwahoji kutokana na ukiukwaji wa taratibu, JamiiForums inadaiwa kuwa ilikataa kutoa taarifa binafsi za mwanachama wake kwa kuamini kuwa chanzo hiki cha taarifa kilikuwa na nia njema hivyo kutaka kwanza iwepo Hati ya Mahakama inayoridhia kukamatwa kwa mhusika na kuelezwa kosa lake.

“MICKE WILLIAM and MAXENCE MELO MUBYAZI on diverse dates between 10th of May, 2016 and 13th day of December, 2016 at Mikocheni area within Kinondoni district in Dar es Salaam Region being the Directors of JAMII MEDIA COMPANY LIMITED operating a social media network commonly known as Jamii Forums as managers and founders , while knowing that the Tanzania Police forces is conducting a criminal investigation on posts containing false information against CUSNA INVESTMENT and OCEAN LINK, published by its members in the said social media network with user names of KWAYU JF Senior —Expert member and AMRISHIPURI, intentionally and unlawfully concealed the identities of said members with intent to obstruct the said investigation.”

 

 

CREDIT: JF

Comments are closed.