Maharage ya nazi na ndizi mzuzu kwa futari
LEO kwenye safu yetu ya Mapishi tutaona jinsi ya kupika maharage ya nazi kama futari ambayo ni matamu kwa kula na ndizi mzuzu zilizoiva.
MAHITAJI:
lMaharage kiasi
lVitunguu
lNazi ya maji nzito kwa nazi moja
lNdizi zilizoiva
JINSI YA KUPIKA:
Chukua maharage, yachemshe mpaka yaive vizuri ukimaliza katiakatia kitunguu, weka tui jepesi la pili, yaache yachemke mpaka kitunguu kiive, ukiona kimeshaiva vizuri weka nazi nzito wengine huita tui bubu.
Liache liive sana mpaka nazi iive lakini uhakikishe yameshikana vizuri, unaweza kuweka sukari kidogo kuleta ladha tamu.
Ukimaliza maharage, kaanga ndizi zako unaweza kula na nyama ya kuku au ya ngombe iliyokaangwa.
Comments are closed.