The House of Favourite Newspapers

Maisha ya Dereva wa Mwalimu Nyerere Yanasikitisha! -Video

0

Mzee Nassoro Rajabu mwenye umri kati ya miaka 80 mpaka 85 ambaye alikuwa ni Dereva wa kwanza wa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere tangu mwaka 1953 mpaka mwaka 1961 wakati wa harakati za kutafuta Uhuru wakati huo alikuwa akitumia gari aina ya Tax yenye nambari za usajili DSO 540.

Gari hio ilikuwa ikimilikiwa na Muhindi, Hata hivyo Baada ya Mwalimu Nyerere kuapishwa na kuwa rasmi kama Rais wa kwanza wa Tanzania, Mzee Nassoro Rajabu aliajiriwa rasmi Serikalini akiwa Dereva wa kwanza wa Baba wa Taifa kuanzia mwaka 1962 hadi mwaka 1985.

Baada ya Mwalimu Nyerere kustaafu aliendelea kumuendesha Rais wa awamu ya pili, Al Hassan Mwinyi, kwa miaka mitatu.

Maisha yake kwa sasa ni duni kwani kula yake ni ya mlo mmoja kwa siku huku akikosa hata godoro la kulalia pamoja na Fedha kwa ajili ya matibabu.

Global TV ilifika kwenye makazi yake ilikujua kinaga ubaga juu ya fumbo la maisha yake, kwanini hana makazi maalumu ya kuishi wakati alijengewa Nyumba na shirika la Nyumba la Taifaa (NHIF) ambapo alifunguka kuwa amenyanga’nywa nyumba.

MSHUHUDIE MZEE HUYO AKITOA SIMULIZI YA MAISHA YAKE YA SASA

Leave A Reply