The House of Favourite Newspapers

Uwoya Apewa Makavu na Mashabiki Kisa Dogo Janja!

0
Staa wa Bongo Fleva, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’, muigizaji wa sinema za Kibongo, Irene Uwoya wakifanya yao.

DAR ES SALAAM: Siku chache baada ya kudaiwa kuwa amefunga ndoa na staa wa Bongo Fleva, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’, muigizaji wa sinema za Kibongo, Irene Uwoya amepewa makavu na mashabiki wenye hasira kali.
Wakizungumza na Risasi Mchanganyiko, mashabiki mbalimbali walisema wanashangazwa na ‘kiki’ anazozitengeneza Uwoya kwani hazina kichwa wala miguu.

 

“Unajua bora angetengeneza kiki na msanii mkubwa ambaye wanaendana hata umri ingeleta maana, sasa Dongo Janja na Uwoya wapi kwa wapi?

Irene Uwoya akiwa katika ubora wake.

“Hata kama Dogo Janja amevuka miaka 18 lakini hawaendani hata kidogo na Uwoya. Uwoya amekubuhu yule, amekuwa kwenye ndoa wakati Dogo Janja yupo shule ya msingi. Uwoya amezaa, ameachika ndiyo aje kuolewa na Dogo Janja?

 

“Haiingii akilini. Hata kama itakuwa ni kweli anatembea naye labda zile za kumega kisela, lakini kimsingi ni anajishushia heshima,” alisema John Katlo, aliyejita-mbulisha kuwa ni mkazi wa Moro-goro.

Msomaji mwingine kutoka Geita, Mwakulakwa Giseni, alisema Uwoya amekosa adabu kutembea na Dogo Janja kwani si saizi yake na ni aibu kwa mwanamke ambaye aliolewa, akazaa na kisha kutembea na kijana ambaye wakati yeye akifanya matukio hayo yote, kijana huyo alikuwa angali anasoma shule ya msingi.

 

Licha ya sakata la Uwoya kuchukua sura tofauti kila uchwao, mwishoni mwa wiki iliyopita Uwoya alizungumza na mwanahabari wetu na kumhakikishia kwamba hajaolewa na Dogo Janja.

 

“Nioelewe nyinyi (Global) msijue?…” alinukuliwa Uwoya na kusisitiza kuwa ile ni filamu.
Uwoya aliolewa mwaka 2009 na mcheza kabumbu wa Rwanda, Hamad Ndikumana katika Kanisa la Mt. Joseph jijini Dar na kufanikiwa kupata mtoto mmoja kisha wakamwagana.

 

Leave A Reply