Maisha ya Sister Fay Kuanikwa Akifariki

STAA wa muziki wa Hip Hop na filamu Bongo, Faiza Omary ‘Sister Fay’ ameibuka na kusema kuwa maisha yake halisi yataanikwa siku ya kufariki kwake kwani ana kitabu anachoandika kila kitu ambacho kitawaacha watu midomo wazi.

 

Akizun­gumza na Ijumaa Wikienda, Fay alisema Watanzania wanayajua maisha yake ya kiki za mjini lakini nyuma ya pazia ana maisha halisi ambayo siku watu wakiyafahamu watashangaa na wapo ambao watabaki midomo wazi.

 

“Nina maisha mengine kabisa ambayo watu hawayajui, nimeandika kila kitu kwenye diary yangu siku nitakayokufa watu watasomewa wasifu wangu watashangaa sana, mimi ni mpambanaji ambaye sijajiweka wazi, kila kitu watu wanaona ni kiki tu,” alisema Fay ambaye kwa sasa amefungua saluni yake kubwa inayoitwa Million Hairs Salon.

STORI: HAMIDA HASSAN


Loading...

Toa comment