The House of Favourite Newspapers

Maiti ya Mtoto Yapiga Kelele!!

0

  maiti ya mtoto (3)Waombolezaji wakienda kuzika mwili wa marehemu, Rahim Fikiri.

STORI: DUSTAN SHEKIDELE, WIKIENDA

Morogoro: Haijawahi kutokea! Kwenye Kijiji cha Melela, Mlandizi wilayani Mvomero mkoani hapa, kumegubikwa na simanzi nzito kufuatia maiti ya mtoto, Rahim Fikiri (2), kukumbwa na mauzauza kibao yakiwemo kupiga kelele wakati wa kuoshwa, mwili kutoka jasho kali na kuliwa macho na masikio.

maiti ya mtoto (2)

MASHEHE WALAZIMIKA

Tukio hilo la kusikitisha lilijiri wiki iliyopita nyumbani kwa wazazi wa mtoto huyo kijijini Melela, Mlandizi hivyo kuwalazimu mashehe kuingilia kati na kushusha dua nzito iliyoondosha mauzauza hayo.

Kufuatia tukio hilo, baadhi ya wananchi wa kijiji hicho walimtonya mwanahabari wetu aliyefika katika kijiji hicho kilichopo umbali wa kilomita 40 kutoka mjini Morogoro ambapo alikutana na msafara wa kuelekea makaburini kwa ajili ya mazishi.

maiti ya mtoto (4)Bibi wa marehemu, Elizabeth Josefu.

BIBI ALIYESHUHUDIA

Akizungumzia tukio hilo, bibi wa marehemu aliyeshuhudia mauzauza hayo, Elizabeth Josefu alikuwa na haya ya kusema:

“Nilipigiwa simu nikaelezwa kwamba mjukuu wangu amelazwa Kituo cha Afya cha Melela. Nilipofika nilielezwa kuwa alipopimwa, alikutwa ana upungufu wa damu.

maiti ya mtoto (1)“Aliongezewa damu na baba yake lakini hali yake ilizidi kuwa mbaya hivyo tulipewa rufaa ya kumpeleka Hospitali ya Mkoa. Tulipofika huko tuliambiwa ana degedege lakini kwa bahati mbaya alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu.

maiti ya mtoto (5)“Tulichukua maiti, tukarejea nyumbani. Tulipofika na kuifunua tukaiona inatoka jasho kali hivyo tukaimwagia maji bakuli mbili.

“Wote tuliogopa tukakimbia, tuliporejea ndani, akatokea paka mkubwa mwenye rangi nyeusi, tukakimbia tena, akaja bibi mmoja hatumfahamu akamfukuza.”

maiti ya mtoto (7)Bibi huyo alisema kuwa, baada ya kuona hali hiyo, yeye na wanawake wenzake walibeba jukumu la kuiosha maiti hiyo ambapo wakati wanamnyoosha mkono wa kulia, marehemu huyo alipiga kelele za mtoto anayelia akilalamika maumivu, jambo lililoibua hofu kubwa hivyo watu wakakimbia.

“Tukio lingine ilikuwa usiku, tulipoifungua maiti tulikuta panya wamekula macho na masikio.

“Baada ya msururu wa mauzauza, wazazi wa marehemu waliwaita mashehe waliosoma dua ndipo hali ikatulia na muda huu tunakwenda kuzika,” alimalizia bibi huyo huku akiangua kilio.

maiti ya mtoto (6)Baba wa marehemu, Fikiri Mrisho

BABA WA MAREHEMU

Kwa upande wake baba wa marehemu, Fikiri Mrisho alipohojiwa na Wikienda alisema: “Inaniuma sana kwani licha ya kumpoteza mwanangu bado anaendelea kuteseka kwa mambo ya kishirikina. Hebu fikiria mwili wake kuliwa na panya! Haya ni mambo ya kutisha.”

maiti ya mtoto (8)NENO LA MWENYEKITI

Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Melela, Yusuf Ally Nguwa alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo alikiri kutokea na kusema serikali haiamini mambo ya kishirikina.

Mtoto huyo alizikwa kijijini hapo huku wengi wakidai mambo hayo ni kawaida kwa Waluguru japokuwa katika tukio hilo hali hiyo ilipitiliza.

Leave A Reply