The House of Favourite Newspapers

MAIZUMO NDOTO YANGU NA MAJUTO IMEYEYUKA !

 

Maisara Mohammed ‘Maizumo’

MTOTO wa miaka minne anayefanya vizuri katika fani ya uchekeshaji, Maisara Mohammed ‘Maizumo’ amesema kuwa ndoto yake ya kufanya kazi na muigizaji mkongwe, Amri Athuman ‘King Majuto’ imeyeyuka baada ya kufariki dunia hivi karibuni.

Akizungumza na Vijistori Mitandaoni, Maizumo aliyejipatia umarufu katika Mtandao wa Instagram alisema, alikuwa anampenda sana King Majuto na alimuomba baba yake amkutanishe naye lakini hakufanya hivyo.

“Nilikuwa nampenda sana King Majuto, nilikuwa napenda kuangalia muvi zake pamoja na matangazo yake, baba aliniambia atanipeleka nikamuone lakini hatukwenda mpaka amekufa,”alisema Maizumo.

Vijistori Mitandaoni lilibahatika kuongea pia na baba yake mzazi, Mohammed Omary ambapo kwa upande wake alisema kuwa siku ya msiba unatokea hakuwa nyumbani lakini aliporudi alimuita Mai nakumwambia kuwa Majuto amefariki lakini chakushangaza alilia sana kama mtu mzima na hata shuleni alikuwa anakataa kwenda, hivyo wakafanya kumlazimisha.

“Ile siku nilikuwa Kigamboni, sasa wakati nafungua mtandaoni ghafla nikaona watu wengi wameposti kuhusu kifo cha mzee Majuto, nilishtuka sana ila baadaye niliporudi nyumbani nikamwita Mai akaja, nikiwa katika hali ya huzuni nikamwambia Mzee Majuto kafariki na hatutamuona tena, lakini cha kushangaza alilia kama mtu mzima mpaka tukajikuta na sisi tunalia, ”alisema Mohammed.

Na Memorise Richard

Comments are closed.