The House of Favourite Newspapers

MAJALIWA AZINDUA X- RAY YA KIDIGITALI KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA RUVUMA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe wakati alipozindua  X-Ray ya kidigitali kwenye hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Ruvuma, Januari 5, 2019.  Kulia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt, Faustine
Ndugulile na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu Mashine ya Kidigitali aliyoizindua katika hospitali ya Mkoa wa Ruvuma kutoka Mtalaam wa tiba ya mionzi (Medical Technologist), Lincleth Gingo kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma mjini Songea, Januari 5,2019. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme na wapili kushoto ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Wtoto, Dkt. Faustine Ndugulile.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisikiliza taarifa ya Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Majura Magafu kuhusu ukarabati wa Jengo la Wakinamama wajawazito wanaosubiri kujifungua katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma mjini Songea, Januari 5, 2019. Wapili kulia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile, wapili kulia ni Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme.
Wananchi wa Songea wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza baada ya kuzindua Mashine ya X-Ray ya Kidigitali kwenye hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Ruvuma, Januari 5, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amezidua  X-Ray ya kidigitali kwenye Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Ruvuma, Januari 5, 2019.

Comments are closed.