The House of Favourite Newspapers

MC Pilipili Amvalisha Pete Mpenzi Wake, RC Makonda Ampongeza

Mshereheshaji Emmanuel Mathias ‘MC Pilipili’ akionesha pete aliyomvalisha mpenzi wake Philomena Thadey (kulia).
…Wakiongea jambo.

USIKU wa kuamkia leo mshereheshaji, Emmanuel Mathias ‘MC Pilipili’ amemvalisha pete ya mpenzi wake (Mke mtarajiwa) Philomena Thadey, nyumbani kwa wazazi wa mwanamke maeneo ya Boko, Tegeta jijini DSM, sherehe hiyo imehudhuriwa na watu mbalimbali wa Serikali na taasisi zisizo za kiserikali.

Alichokisema Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda baada ya MC Pilipili kumvalisha pete mpenzi wake

😷😷😷😷🙄🙄🙄🙄🙄. Sipati picha waleeeeeeeeee waliokuacha wanavyokutazama. Mmoja eti anasema unaigiza. Nakuomba mc Pilipili umsaidie na @diamondplatnumz kwani yeye kila tarehe ikikaribia anasogeza mbele ona sasa anamsubiri Rick Ross aje, sasa sijui ni harusi au Tamasha, heri ya @majizzo ameamua kufungia China sasa tunasubiri send off huku, balaa lipo kwa @lemutuz_superbrand kila siku anaachwa yaani kimsingi mji huu ndio pekee watu wanaanza Honeymoon kabla ya kufunga Ndoa.


Comments are closed.