The House of Favourite Newspapers

Majaliwa Mgeni Maadhimisho ya Ualbino

1
Mwenyekiti wa Chama cha Watu wenye Ualbino Tanzania (TAS), Names Temba.

Na Gabriel Ng’osha/GPL

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uelewa Juu ya Ualbino yatakayofanyika Juni 13, mwaka huu mkoani Dodoma.

Akizungumza na Global TV, Mwenyekiti wa Chama cha Watu wenye Ualbino Tanzania (TAS), Names Temba, alisema maadhimisho hayo ambayo ni ya 12 kitaifa na ya tatu kimataifa,  yana lengo la kutoa elimu zaidi juu ya uelewa kuhusu ualbino ambapo kauli-mbiu yake itakuwa “Takwimu na Tafiti Kwa Ustawi wa Watu Wenye Ualbino”.

“Kama TAS tumejipanga kutoa elimu ya uelewa kwa wananchi kuhuu ualbino, kinga na tiba kwa saratani ya ngozi ambayo imekuwa ni changamoro kwetu, kutoa mafuta-kinga kwa ajili ya kuzuia mwanga wa jua, kofia pana, miwani ya jua, miavuli, kliniki ya sheria kwa waathirika wa matatizo mbalimbali kwa watu wenye ualbino na midahao kutoka Taasisi za Haki za Binadamu, Sheria na zinginezo.

“Mgeni rasmi kwenye maadhimisho haya ni Waziri Mkuu Majaliwa na tunatarajia kuwa na baadhi ya wasanii likiwemo kundi la muziki la Tanzania One Threather (TOT).

“Vilevile tumewaomba wadau wa vyombo vya habari na wengine kutuunga mkono katika kukamilisha maadhimisho hayo,”alisema Temba.

 

1 Comment
  1. […] akiwa na ulemavu wa ngozi. Baaye anapata ulemavu wa […]

Leave A Reply