The House of Favourite Newspapers

Majaliwa: Rais Dkt. Samia Amedhamiria Kuendeleza Sekta Ya Kilimo

0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeweka msisitizo katika kuendeleza Sekta ya kilimo kwenye mazao ya chakula na Biashara.

Amesema lengo ni kuhakikisha nchi inajitosheleza kwa chakula na kila Mtanzania anayejishughulisha na kilimo aweze kukuza kipato chake na uchumi Taifa kwa ujumla.

Amesema hayo Disemba 29,2023 wakati akizungumza na wakazi wa kijiji cha Juhudi B kwenye kata ya Chinongwe, Ruangwa mkoani Lindi.

Amesema Rais Dkt. Samia wakati wote amedhamiria kuhakikisha Tanzania inakuwa kimbilio la wengine wanaohitaji mazao “Tumuunge mkono Rais wetu kwenye mapambano yake ya kukuza sekta ya kilimo, amefanya makubwa kwenye sekta ya kilimo ikiwemo kuagiza kutengwa kwa maeneo ya kilimo kwa ajili ya vijana”

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameongeza bajeti kwa ajili ya ujenzi wa barabara za ndani katika wilaya ya Ruangwa kutoka shilingi Bilioni 1 hadi shilingi bilioni 4.8

“Niwape Siri, Rais Dkt. Samia ametuunganisha Masasi na Ruangwa kupitia ujenzi wa barabara ya Nanganga-Ruangwa na Km 38 zimejengwa pia ametupa fedha kwa ajili ya kuunganishwa Ruangwa na Nachingwea kwa kiwango cha lami”

 

View this post on Instagram

 

A post shared by OFISI YA WAZIRI MKUU (@owm_tz)

Leave A Reply