The House of Favourite Newspapers

Majembe Mpya Yanga Kutua Julai 10

0

KUANZIA Julai 10, mwaka huu, tunatarajiwa kuyaona majembe mawili mapya ya Yanga kutoka Rwanda na DR Congo yakitua hapa nchini kwa ajili ya kujiunga na timu hiyo.

 

Hatua hiyo imekuja baada ya nchi hizo kuwa mbioni kufungua mipaka yao baada ya kuifunga kwa muda mrefu kipindi hiki cha corona.Baada ya mipaka ya nchi nyingi kufungwa katika kujilinda na corona, Yanga ilishindwa kumalizana na winga Tuisila Kisinda anayekipiga AS Vita ya DR Congo na beki wa kushoto kutoka Rayon Sport ya Rwanda, Eric Rutanga.

 

Taarifa mpya ni kwamba, mipaka ya Rwanda inatarajiwa kufunguliwa Julai 10, huku ile ya DR Congo ikifunguliwa Julai 15, hivyo majembe hayo itakuwa muda muafaka kwao kutua hapa nchini.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Tuisilia alisema: “Kila kitu kuhusu usajili wangu wa kujiunga na Yanga ulikuwa unaenda vizuri lakini shida ilikuwa kutofunguliwa kwa mipaka ya hapa nchini kwetu ila baada ya kufunguliwa mipaka nitakuja Tanzania au viongozi wa Yanga watakuja huku Congo kukamilisha dili langu.

 

”Kwa upande wa Rutanga ambaye hivi karibuni alitumiwa mkataba kwa njia ya e-mail, alisema: “Nilikuwa katika wakati mgumu kuona dili langu la kutua Yanga linachelewa baada ya mipaka kufungwa, nimefurahi kusikia Julai 10 mipaka itafunguliwa, hivyo ndoto yangu ya kuichezea Yanga inaenda kutimia.

MARCO MZUMBE,Dar es Salaam

Leave A Reply