The House of Favourite Newspapers

Lungi Alia na Wanaume wa Watu

0

STAA wa sinema za Kibongo, Lungi Mwaulanga ameibuka na kutoa kilio chake baada ya kuumizwa na wanaume wa watu kufuatia jinsi walivyomtenda.

 

Akipiga stori na Risasi Vibes, Lungi alisema, wanaume hao wa watu ni wanyanyasaji, hivyo kuwataka wanawake wenziye wasiingie mtego kama alioingia yeye.

 

“Wanaume wa watu si wanaume, anakutumia tu kisha anakubwaga. Nadhani nikipata kibenten nitakuwa na amani, lakini nikagundua hata wao wana shida zao, mastaa wengi ‘wana-date’ na vibenteni wakidhani watafarijika, lakini nao wanasumbua sababu wanataka maisha yao mengine.

 

“Kibenteni naye hata umpe nini, hawezi tulia mazima kwa sababu naye anataka haki ya kuwa na mwenza anayeendana na yeye, mi natoa somo kwa wanawake wenzangu kujituma na kusubiri wenza wa maisha na siyo mume wa mtu wala kibenteni, wote ni sawa tu,” alisema

Leave A Reply