The House of Favourite Newspapers

Majibu ya DNA ya Naomi kutoka kesho

Image result for marehemu Naomi Marijani

WAKATI familia ikiwa inategemea majibu ya DNA ya marehemu ndugu yao, Naomi Marijani, yatoke leo, hali imekuwa tofauuti baada polisi kutoa tamko kwamba hawajaridhishwa na ripoti iliyotoka, hivyo wanaomba ndugu wawe wavumilivu kwani kesho asubuhi majibu hayo yanaweza kuwa tayari.

Akizungumza na mwandishi wa habari leo, kaka wa marehemu, Wiseman Marijani, alisema kuwa wao kama familia tayari walishajipanga kwa ajili ya kufanya msiba, lakini kama jeshi la polisi limesema halijaridhishwa na majibu na kuwataka wawe wavumilivu, basi hawana jinsi zaidi ya kuwa wavumilivu.

“Unajua sisi kama familia tulishajipanga kwa ajili ya kuweka msiba kwa sababu tuliambiiwa leo saa nne asubuhi tunapatiwa majibu ya DNA ya ndugu yetu, lakini cha kushangaza ni kwamba tumeambiwa kuwa polisi hawajaridhishwa na ripoti iliyotoka, hivyo tuwe wavumilivu mpaka kesho asubuhi,” alisema

Stori: Memorise Richard

Comments are closed.