The House of Favourite Newspapers

Majimaji Yataja Kinachowabania Pointi Ligi Kuu – Video

0

BAADA ya kuwa na mwanzo mbaya katika Ligi Kuu ya Vodacom, Majimaji sasa imesema inajipanga kuamka na kufanya vizuri huku ikitaja uwanja wao wa nyumbani ni sehemu ya kikwazo cha wao kutofanya vizuri.

Akizungumza juu ya mwenendo wao wa ligi ambapo hadi sasa Majimaji inayodhaminiwa na Kampuni ya Sokabet ikiwa inashika nafasi ya 14 kati ya timu 16 za ligi hiyo, Ofisa Habari wa Majimaji FC, Onesmo Ndunguru amesema kuwa benchi la ufundi liko bize kufanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza na wanaamini ndani ya muda mfupi timu yao itaamka na kufanya vizuri.

Ofisa habari huyo amesisitiza kuwa timu yao inapokuwa ugenini imekuwa ikicheza vizuri tofauti na inapokuwa nyumbani jambo ambalo wamebaini kuwa yawezekana uwanja wao wa nyumbani wa Majimaji mjini Songea umekuwa kikwazo kwao lakini chini ya makocha Peter Mhina na Habib Kondo wanajipanga kufanya vizuri.

Ndunguru alizungumza hayo kabla ya mchezo waoa uliopita dhidi ya Lipuli ambapo alisema: “Tuko vizuri, kikosi kina ari lakini tunapokuwa nyumbani hatufanyi vizuri, tumegundua kuwa uwanja wetu umekuwa ukitukamata sisi wenyewe lakini hilo tunalifanyia kazi.”

Ofisa huyo wa habari hakufafanua ni kwa jinsi gani uwanja wao wa nyumbani umekuwa ukiwabana wao wenyewe kupata ushindi.

Mchezo ujao timu hiyo inatarajiwa kukutana na Mwadui FC kwenye Uwanja wa Majimaji ulipo katikati ya Mji wa Songea mnamo Jumapili ya Oktoba 29, 2017.

Majimaji ambayo ilisaini mkataba wa mwaka mmoja na Sokabet, kampuni ambayo inajihusisha na michezo ya kubashiri matokeo imekuwa haina matokeo mazuri, kwani katika michezo saba ya ligi kuu, haijashinda hata mmoja, sare nne na imepoteza michezo mitatu.

Na Mwandishi Wetu.

Usipitwe na Matukio, Install App Yako ya Kijanja na Namba Moja Tanzania ya Global Publishers

Android Bofya ===> Google Play

iOS Bofya ===>Apple Store

VIDEO: Ofisa Habari wa Majimaji FC, Onesmo Ndunguru Akifunguka

Leave A Reply