The House of Favourite Newspapers

“1ST HOUSING FINANCE” KUTOA MIKOPO NAFUU YA NYUMBA

0
Mkurugenzi Mwendeshaji wa 1st Housing Finance, Omar Msangi, akizungumza jambo katika hafla hiyo.
Kiongozi mshiriki katika kampuni hiyo, Simon Grgary, akizungumza jambo.
Hafla hiyo ikiendelea.
Mjumbe wa Menejimenti ya Utendaji na Ofisa wa Mahusiano ya Uwekezaji, Conrad D’souza, akizungumza jambo.Mjumbe wa Menejimenti ya Utendaji na Ofisa wa Mahusiano ya Uwekezaji, Conrad D’souza, akizungumza jambo.

 

KAMPUNI ya kwanza ya utoaji wa mikopo ya nyumba nchini iitwayo 1st Housing Finance (Tanzania) Limited yenye makazi yake Upanga jijini Dar es Salaam leo imezinduliwa rasmi.

Kampuni hiyo imeanzishwa na Bank M ikishirikiana na International Finance Corporation (IFC) kampuni inayoongoza katika sekta ya mikopo ya nyumba barani Asia ambapo washiriki wengine wakiwa ni familia ya Kamimjee na Sanjay Suchak.

Kampuni hii ilipata leseni kutoka Benki Kuu Julai 18 mwaka huu kufanya shughuli zake chini ya sheria ya taasisi za fedha na mabenki ya mwaka 2006 na ilisajiliwa na Brela chini ya sheria za nchi na mtaji wake ni Shilingi 21.80 Bilioni.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mwendeshaji wa kampuni hiyo, Omar Msangi, alisema Benki M imeshirikiana na washirika wanaoheshimika kimataifa kama vile IFC na Housing Development Finance Corporation Limited (HDCFC) na familia zinazoheshimika kibiashara nchini wakiwa na mtazamo wa kuingia katika soko la mikopo ya nyumba.

“Kampuni hii ni ya kwanza kujikita kwenye sekta ya nyumba za makazi na inakuja na suluhisho la muda mrefu la makazi kwa Watanzania na suluhisho la riba nafuu kwa wateja wao,” alisema Msangi.

Aliendelea kueleza kwamba 1st Housing ambayo ni ya kwanza hapa nchini katika soko la mikopo ya nyumba za makazi, itaanzia kutoa mikopo ya aina nne ambayo ni mikopo kwa ajili ya ununuzi wa nyumba, mikopo kwa ajili ya ukarabati wa nyumba, mikopo kwa ajili ya upanuzi wa nyumba na mikopo kwa ajili ya kununua nyumba nyingine kwa kutumia thamani ya nyumba yako.

“Kingine kitakachotutofautisha kwenye soko hili ni kutoa mikopo ya muda mrefu hadi miaka 20. Hii itarahisisha ulipaji wa mikopo kwa mwezi kuwa rahisi na hivyo kipato cha mwezi cha mkopaji kutosheleza kufanya mambo mengine ikiwa ni pamoja na maombi ya mkopaji kushughulikiwa ndani ya saa 24,” alisema.

NA DENIS MTIMA/GPL.

Usipitwe na Matukio, Install App Yako ya Kijanja na Namba Moja Tanzania ya Global Publishers

Android Bofya ===> Google Play

iOS Bofya ===>Apple Store

Leave A Reply