The House of Favourite Newspapers

Majina ya watakaounda baraza la mpito kwa Haiti yawasilishwa

0

Viongozi wa nchi za Karibiani wanasema makundi yote na vyama vya kisiasa, isipokuwa kimoja, vimewasilisha majina ya watu walioteuliwa kwa ajili ya baraza la mpito la rais, lenye jukumu la kuchagua waziri mkuu wa muda wa Haiti, nchi ya Caribbean inayoendelea kugubikwa na ghasia za magenge.

Baraza la awali la wanachama tisa lilipunguzwa hadi wanachama wanane, baada ya chama cha Pitit Desalin, kinachoongozwa na seneta wa zamani, na mgombea urais Jean-Charles Moise kukataa nafasi hiyo.

Kundi llililoundwa Desemba tarehe 21 lililoshirikiana na Waziri Mkuu Ariel Henry lilikuwa mojawapo ya waliochukua hatua katika siku za mwisho likiwasilisha jina la mwakilishi wake juzi Jumatatu.

Rais wa Guyana Irfaan Ali alisema kuwa jumuiya ya kibiashara ya kikanda ya Caricom imekuwa ikikutana karibu kila siku kusaidia kuunda baraza hilo.

MRITHI wa ZITTO KABWE DOROTHY SEMU AKITANGAZA MABADILIKO MAKUBWA NDANI ya ACT na UCHAGUZI…

Leave A Reply