The House of Favourite Newspapers

Makabila: Simuogopi Nay wa Mitego, Namheshimu na Naweza Kumvunjia Heshima Pia

0
Nay wa Mitego

MSANII wa Singeli Bongo, Dullah Makabila amemjibu Nay wa Mitego baada ya Rapa huyo kutumia ukurasa wake wa Insta story yake kusema kuwa wasanii wengi wa Singeli hawajielewi huku akimtolea mfano Dullah makabila kuwa ni moja ya ambao hawajielewi,kichwani ni zero.

 

Hii inakuja baada ya msanii Makabila kuandika walaka mrefu sana wa kuomba radhi kwa msanii Diamond Platnumz ili amrejeshe tena kwenye familia ya Wasafi.

Dullah Makabila

Kupitia Empire ya EFM, jana Juni 6, 2022, Makabila amedai Nay ni kaka yake lakini anapaswa kujua kuwa anamuheshimu na sio kuwa anamuogopa, hivyo anaweza kumvunjia heshima muda wowote na kama angekuwa na busara basi angemfuata private kumwambia amekosea na sio kwenda kumtukana hadharani mitandaoni.

 

Makabila pia amemtaka Nay wa Mitego amuombe msamaha haraka, Dullah ameongeza pia kwamba anaamini hakuna baya alilofanya na wanaoona amekosea wana chuki binafsi na Diamond.

Leave A Reply